1.
MUNGU MKUBWA hana choyo. Yeye amemjaalia kila
mtu aliyekamilika, kuwa na uwezo na ujasiri wa kuyakabili magumu kwa uvumilivu
na subira na mwishowe kuibuka akiwa mshindi.
2.
Katika kupanda, kuotesha, kupalilia na kuwekeza
mbegu ya harakati ya kujiweka huru, au kuondoa bendera ya uhuru wa wachache
wanaowatia utumwani walio wengi, kutokata tamaa ndiyo moyo unaosukuma damu ya
mafanikio.
3.
Cha
msingi ni kuweka nia pamoja na mikakati ya kujinasua bila kuzembea, iwekwe
jitihada kunyanyua mguu, kukata myororo, kuvunja pingu na kupiga hatua kuelekea
kwenye ngome za wakandamizaji na kuwapokonya silaha za domo na za ujuzi wote.
4.
Kunahitaji
moyo Na ujasiri WA kuyaendeleza matokeo mazuri ya kutoka minyororo hadi
kuwazingira waliotuweka zizini wakatufanyisha kazi kiroho na kimwili pasipo
sisi kujitambua;ni hawa wanefili wenye sifa na akili za giza, watoto wa
muharibifu shetani,wanao kula nyama na damu za watu,na kuwafanya wengine
watumwa milele kwa njia ya elimu dunia.
5.
Leo
watu wengi wamekuwa maskini saana duniani, na wanakufa kwa njaa pia magonjwa ya
ovyo;ijapokuwa Muumba wa mbingu na dunia amefanya yote bora, ili mwana adam
arizike na ardhi aliyowekwa aitawale.
6.
Mbona
itakuwa misharabaka mikubwa,wakati maskini,watajitokesha ndani ya shimo zao za
ufichoni na kuwashambulia watawala wa dunia hii kwenyi magorofa ya ustarehe
wao,ili wapate maji masafi na mkate wa kula.Itakuwa mwanzo wa vita vya
mwisho,duniani;kwani vita vya ARMAGIDONI ni vita vya kiroho,yaani vyaa
makanisa,pia vita kati ya matajiri na wa maskini. Sela.
7.
wakimbizi
wanaoweza kuswagawa na kufanikiwa kuwadhibiti wasiwepo nchini. Wapo mamilioni,
wanachotakiwa ni kujipanga safi na kusonga mbele kwa namna itakayowatatiza
wasifanye uharibifu wananchi pale wanapozuia sahani ya mlo isiwaondoke.
8.
Munanyanyasa
wakimbizi leo na wageni ;kesho mutakuwa wakimbizi,hadi kwa inji za
juu ;mbalamwezi na nyota zitawapokea na hamutaonaka dunia hii takatifu
tena.Kwani katika dunia zisizo onekani zilizo nyingi kama ma elfu ;hamna
hewa,mwangaza,wala udogo wa mibaraka ;kama dunia aliyopewa ADAM na
HAWA.Nayo maficho ya bustani la EDENI,ni uel mji wa baraka,tokea mlima wa
Abale ;muwe mukijua.
9.
Wakati
wa kubariki pembe ine za dunia munaimba wimbo huu ; « WATU WA
INCHI ZINGINE,WATAKUJA SHUHUDIA »Wakati wa kusonga mbele wimbo uwe,
"Ninaye Mungu Mukubwa AHMIRADO,jemadari wangu,atashinda vita".
10. Lengo kila mchaguliwa aelewe kuwa kukata tamaa
ni sawa na kukaza kitanzi(Kamba) shingoni. Ni sumu inayoua akili na moyo
vifanye jitihada za kujing'oa kwa makucha.
11. Songa mbele tu,na songa ugali kubwa na mchuzi
nzuri,ukipata ule mda na ile bahati ;sababu,wakati adui
atakuja ;atakuteka nyara na utaacha chungu chako jikoni,kiliwe na
umbwa.Karamu na karamu,ziwe kwako siku zote,utakapo kumbuka ukombezi wako wa
tarehe 28 na tariki 3 mwezi wa 6.
12. Kiasili muhimu katika kanisa la upendo
itakuwa,kunona kwa binti na wavulana wako.Usafi wa watoto na wazee wako,uzuri
wa nyumba na mahali munapokaa,bonde za maua na nyimbo za kudondoza roho,pia
kusisimua nywele.Sela.
13. Mchaguliwa hakutumwa kushindwa ku dunia.hata
katika michezo za kandana na mitihani za shule, ao zoezi zingine ;awe kwa
mustari za mbele tu.Bila hivyo ;ni aibu kubwa sana mno.
14. Kila
mtu, atafurahia utamu wa matunda ya mafundisho ya kitabu chenyi mihuri
saba ;naye atauzingatia saana katika moyo wake,ili atembee kwa njia aliyo
amuriwa.Ni ndani yake njoo wafalme wa dunia itakayokuja na wakubwa wengine
wote,watatoke.Muwe mukijua.
15. Bendera iliyo simamishwa mbele yenu,toka
mbingu ya tatu,aliyoshuka nayo,baba mtukufu ;ni bendera ya upendo.Moyo
wakujitolea na damu iliyo mwangika ajili ya ukombozi wa wengine watu.Mujue
kujitolea sasa.Dunia ni ya mda mfupi.
16. Wachaguliwa wana nguvu, wakiamua wanaweza
kuitumia kujitia utumwani wakikata tamaa kwa kudhani kuwa ni Mungu Mkubwa ndie
anayetaka wawe hivyo chini zaidi.Kumbe ni kusitasita njo inawakasesha vyote.
17. Ikidhaniwa Mungu ndiye anayewadumisha kwenye
viti viongozi wa utawala usiojali wananchi itakuwa ni kumsingizia. Si Yeye
anayewatia njaa, umaskini, maradhi na ujinga. Maana ameweka kanuni kuwa
mwananchi hatovuna ila kile alichokitolea jasho na atayaona matunda yake.
18. Ni katika kanuni hii tunawakuta wazee wa watu
weusi wameibuka na ushindi dhidi ya ukandamizaji wa watu weupe,kwa njia ya
uhuru. Hata watu weupe, walikuwa na vita vyao vya maendeleo, kwakuvunja
minyororo ya utawala wa kimabavu na ujinga,ili leo wajisikie wana tulia ki
maisha na kiuchumi.
19. Walifanya jitihada za kuamshana mpaka wote
wakatambua dhuluma waliyotendewa haikupangwa na Mungu. Wakawaambia mabwanyenye
wa kikoloni kuwa mmetunyonya vya kutosha. Sasa tunataka jasho la kodi zetu
lijenge na kuboresha afya za wananchi, nasi tupatiwe mlo kamili. Mapato ya
utalii, madini, misitu, kilimo, uvuvi na viwanda yabadili vidungu (misonge)
tunavyoishi ziwe nyumba.
20. Ile hali ya kusema 'sawa Bwana mkubwa'ndio
padri’ na kuwatungia nyimbo, wanyonyaji wa kikoloni wakaikomesha.Lakini
tukijitathmini tulivyonufaika wananchi tangu wazungu waliposhusha bendera na
kufunga virago vyao. Uhuru ule uliopatikana kwa jasho la babu zetu umetekwa
nyara na 'wenzetu' wachache.Makanisa zimedanganya saana kuliko chama cha
wafanya siasa.Kwa hivyo, tutumikie kanisa moja tu ya kweli ;ni kanisa la UPENDO
tu.
21. Hata huko awali, walikuwepo wasaliti
waliowapiga bei wafalme na makuhani wakubwa wao,hata manabii walisalitiwa na
ndugu zao wa karibu.Wachaguliwa wa sasa, Mungu Mkubwa atuhurumie,ile kikombe
isitufikie,moyo mgumu ule,mpaka tumtoe mwana kondoo tena,ashindwe kufanya kazi
yake. « SHANGWE KWAKO MWANA KONDOO,KWAKUTUFIKISHA SAYUNI ».
22. Kuna wananchi wasiopenda amani wanaotaka
kuleta vurugu.Katika kila jambo, wanatafuta mizozo na fujo tu. Nyinyi musiwe
hivyo, muegemee tu upande wa haki na kweli.musifuate sauti ya walio wengi
tu,mara nyingi,inapoteza raia wapumbafu. Ni heri kuwa na mtawala mkali, kuliko
kuwa na mtawala muongo.
23. Je, wanaochangia maji ya mshimu na ng'ombe ao
nguruwe mtawaelezaje. Mtawaambia nini wanaopata maji ya bomba katika jiji,na
mwishowe yaonekana kama maji yana vidudu na kugonjwesha watu ?. Mtawaambia
nini eeh watawala, wakati chanjo zenu za kukingia maradhi,zageuka sumu kwa
watoto na kuzagaa ukimwi kwa makusudi kwa maskini wa afrika na wa arabu.(hii ni
ufunuo).

Baba mtukufu,
Mwangaza wa dunia.
Bujah 25/05/2008
click here for a query
No comments:
Post a Comment