Tuesday, March 1, 2016

KITABU CHENYI MIHURI SABA / KANISA LANGU,KANISA LANGU

               KITABU CHENYI MIHURI SABA / KANISA LANGU,KANISA LANGU
KANISA LANGU NI ROHO YANGU,KANISA LANGU NI UMOJA WETU,SISI TUNAO AMINI KWELI NA HAKI.
KANISA LANGU NI LA WAZIMA NA WAFU WALIOTAKASWA.KATIKA KANISA LANGU HAKUNA LAWAMA YA DINI WALA YA KABILA.KANISA LANGU NI KANISA LA DAMU ILIYO TAKASWA,DAMU YA BABA UMOJA,ALIYEUMBI MBINGU NA INCHI,KUPITIA KIMVULI CHAKE SOTE TUMEUNGANISHWA,KANISA LANGU KANISA LANGU.KANISA LANGU SIO NYUMBA WALA KITABU;KANISA LANGU NI UKWELI WA SIKU KWA SIKU ZINAZO ENDELEA KATIKA ULIMWENGU.KANISA LANGU LINAAMINI ELIMU NA KUIPINGA PIA KAMA INALETA KUJIPENDELEA NA KUANGAMIZA.KANISA LANGU NI KATISA LA UTOWAJI,UTOWAJI WA SADAKA,SADAKA YA KUTUKETESWA,MIMI NA WEWE NA YEYE NA SISI,TAYARI KUFIA NENO NA MUSIMAMO WA IMANI YETU MPAKA MWISHO.KANISA LANGU NI KANISA YA MIUNGU MIDOGO YAANI –KA-N-ISSA.MAAN YAKE MAKAO YA MIUNGU MIDOGO.ISSA KATIKA LUGHA YA MBINGUNI NI MUNGU MDOGO.KA NI MAHALI (N)NI ANAPOKAA AO WANAPOKAA,ISSA NI MIUNGU MIDOGO.
KANISA LANGU NI MAMA WA MAKANISA.WOOTE WANAO AMINI ,PAMOJA NA VIUMBE VYOOTE VINAVYOISHI,NI WANAMEMBA WA KANISA LANGU.VINAVYO ONEKANA NA VISIVYO ONEKANA NI VIUNGO NDANI YA KANISA LANGU.KANISA LANGU HALIHUBIRI CHUKI WALA MATUSI AJILI YA IMANI ZINGINE,HATA KAMA IMANI ZINGINE HIZO ZIKO FEKI.UFEKI WA IMANI ZINGINE,UNATUPA SISI NGUVU YA KUTAMBUWA UKUBWA WAKE ALIYE TUHUBIRI NA BILA UFEKI WA MAIMANI ZINGINE,TUTAFUNDISHA NINI?SHERTI WAZAIFU WAWE KATIKA DUNIA ILI WENYI NGUVU WAONEKANE.
KANISA LANGU NI LA UTAKATIFU,NDANI MNA WATAKATIFU KWELI WATENDA ZAMBI NA WAJITAMBUAO UZAIFU WAO.KATIKA KANISA LANGU  WATU WOTE NI KAMA SAWA-SAWA.KATIKA KANISA LANGU KUNA MATAJIRI NA WA MASKINI,KUNA WAKAMILIFU NA WAZAIFU PIA,ILE YOOTE NI MPANGO WA MAUMBILE YA KILA MTU TANGU MWANZO,PIA MPANGO MUHIMU YA UFALME WA MUNGU MKUBWA HAPA KUDUNIA.
KANISA LANGU NI SHULE LANGU LA MSINGI,PIA NI CHUO KIKUU (UNIVERSITE)KWANGU MIMI NA KWA DUNIA NZIMA.KANISA LANGU NI HOSPITALI KWA MWILI NA ROHO YANGU,NI SOKO NA DUKA MAHALI MIMI NAPATA KILA KITU NINACHO HITAJI.KANISA LANGU PIA NI GEREZA LANGU,MLE NAPATA KIFUNGO PIA MALIPIZI YA ASILI YA UBAYA NILIYO ZALIWA NAYO,NA HII INAFANYIKA KWA NJIA MBALIMBALI,KIWAZI NA KISIRI KADIRI YA MAPENZI YA MUNGU MKUBWA WANGU;KANISA LANGU,KANISA LANGU.
KANISA LANGU NI LA AJABU,LIMEANZIA NDANI YA MWILI WANGU NA KUINUKIA NDANI YA NYUMBA YANGU,WAKIWEMO MIMI KAMA MUHUBIRI,MKE AO WAKE WANGU KAMA MUOMBAJI AOWAOMBAJI ,NA WATOTO WANGU WAKIWA WAIMBAJI NA WAHUDUMU KWA KAZI MBALIMBALI.
MUUMBA WA MBINGU NA DUNIA ANASEMA KILA SIKU KINYWA KWA KINYWA NDANI YA KANISA LANGU.YOOTE NINAYOFANYA NAIFANYA KUPITIA AMRI ANANIPA MUUMBA WANGU AKIPITIA NJIA MBALIMBALI.KWA ZAMIRI SAFI ,KWA KUONA NA KUIKIA,KWA NDOTO ZA MCHANA NA NDOTO ZA USIKU.NDOTO MCHANA NI MAWAZO NINAYOPANGA NIKIWA SILALI,NA NDOTO ZA USIKU NA NJOZI NINAZO OTA NIKIWA KATIKA USINGIZI MZITO,KWA MAFUNDISHO YA KITABU CHENYI MIHURI SABA PIA BIBLIA TAKATIFU.NINAONGOZWA PIA KWA NJIA YA ULEVI WA IMANI.YAANI KUJAZWA KWA WAPANDA FARASI NDANI YA JAMAA TAKATIFU.MWISHOWE KATIKA KANISA LANGU;MUUMBA WA MBINGU NA DUNIA ANATUMA SAUTI KUJA KUTUONGOZA.NA HIYO INAFANYIKA KWA RUHUSA TU YA KIMVULI CHAKE,APANA KWA RUHUSA YA MTU MWENGINE YEYOTE YULE KATIKA DUNIA KWA AJILI YA KUCHUNGA UMOJA WA WACHAGULIWA .SELA.
KINISA LANGU NI LA AJABU PIA LA ISHARA.KATIKA KANISA LANGU,HATA WAFU HAWAKUFE NA KUNYAMANZA KIMYA,ILA WANABADILIKA TU NA KUENDELEA KAZI ILEILE WALIOKUWA WAKIFANYA AO KUONGEZEWA KAZI ZAIDI YA HIYO.KANISA LANGU,KANISA LANGU.
KANISA LANGU MNA MANENO MAZITO SAAANA YALE ALIPASHWA TU FUNUA ROHO MTAKATIFU PEKE YAKE.KATIKA KANISA LANGU;KUMEFUNULIWA MAMBO SABA MAKUBWA,ILIYO MIHURI SABA ALIYOVUNJA KRISTU WA LEO.NA MANENO HAYA NDIYO IFUATAYO:
1/SHETANI HAIKO MBALI,NI MWILI WA MTU NA ZAMIRI ZAKE.SIYO KITU KINGINE.
2/ZAMBI HAZIKO.ZAMBI NI KILE TU HAKIRUHUSIWI NA SAUTI YA MUNGU MKUBWA.
3/YESU HATARUDI MAWINGUNI KAMA VILE ILIANDIKWA KI MWILI.TAYARI ALISHA ZALIWA NA ANAENDELEA KUZALIWA KILA KIPINDI KWA NJIA MBALIMBALI KUPITIA MANYOTA.
4/WAFU HAWALALI.WAFU NI WAZIMA.WANAZALIWA TENA KU DUNIA.
5/MALAIKA HAWANA MABAWA.NAO NI WATU NA WENGI WANAISHI KU DUNIA.
6/MUNGU NI MWANAMKE.KWANI NI YEYE ANAYEUMBA.AKITAKASWA DUNIA INAOKOLEWA.
7/UFALME WA MUNGU DUNIANI KAMA VILE MBINGUNI UNAPASWA KUANZIA KWA WATU WACHACHE,NAO WANAIPANUA DUNIANI POTE.NA UFALME HUO UNAANZIA KUPITIA KARAMU YA MWISHO NA DAMU YA BABA MTUKUFU.NA HII NJO JAMAA TAKATIFU YA KWELI,MUWE MUKIJUWA.
KANISA LANGU LINAWATUMA NJIWA AO MAKINDA TAKATIFU KWENDA KUONA KAMA MAJI YAMEKAUKA NA KULETA RIPOTI KWA NOA ALIYE BABA MTUKUFU.YAANI MUNGU MKUBWA ANATUMA WATU WAENDE SOMA MASOMO YA KIMWILI AO YA KIROHO,KATIKA MAKANISA ZINGINE WALA MAELIMU MBALIMBALI ZIBAYA NA ZIZURI,ILI WALETEE WACHAGULIWA USHUHUDA NZURI AO MBAYA AJILI YAKUJENGA IMANI YA JAMAA TAKATIFU.LAKINI WASIO WACHAGULIWA KAMILI,WANAENDA NA HAWATARUDI.WATAANZA KUTUKANA IMANI YA JAMAA TAKATIFU AJILI YA TUMBO YAO AO TAMAA YAO MBAYA NA HII ILIANDIKWA SIO MUSTUKO.KANISA LANGU,KANISA LANGU.
KATIKA KANISA LANGU,UPENDO NJO MUNGU MKUBWA,NJO JINA LA MUNGU WANGU,NJO MAHUBIRI NA IMANI YANGU,NJO MWANZO NA NJO MWISHO,PIA NJO KIFO NA UZIMA.KWA MAANA UPENDO UNAUWA.NA UPENDO UNA PONYA.UKIPENDA SAANA UTAKUFA NA MAPENDO NA UKIPENDA VIBAYA UTAKUFA VILE VILE.PENDA KADIRI YA MAPENZI YA MUNGU MKUBWA.YAANI PENDA ANACHOPENDA YEYE WALA USIPENDE KITU KINGINE,HATA KAMA MUUMBA WAKO ANAKUPITISHA NDANI YA MTIANI KUONA KAMA UMEKWISHA KU KAMILIKA.
ZAMBI YA ADAMU NA EVA,YAANI ZAMBI YA DAMU NA MWILI,ILIKUWA ZAMBI YA MAPENDO,ILIYO GEUKA MAPENZI,KINYUME NA MAPENZI YA MUNGU MKUBWA NA IKALETA KIFO NA KUJUWA SANA KWA MWANAADAMU.BASI UJANJA UKAINGIA DUNIANI,UPINGAJI NA MALUMBANO.WATU KUANZA KUBISHA NENO KUTOKA KINYWA CHA MUNGU MKUBWA NA KUUNDA VIKUNDI VYA  UPENDO CHAFU YA KUHARIBU MJI NA KANISA LA MUNGU ALIYE HAI MPAKA KULETA LAANI DUNIANI.YAANI RAHA ITAKAYOPITA,NA KUSAHAU MSINGI WA MUNGU MKUBWA KUUMBA MTU NI AFANANE NAYE,AWE MUNGU MDOGO NA ZAMBI ZIISHE ILI UFALME UMILIKI KILA KITU KU DUNIA.KANISA LANGU,KANISA LANGU.
 
IMEANDIKWA NA BABA MTUKUFU,KIMVULI CHA MUNGU MKUBWA BABA WA IMANI.SAUTI YA MNYONGE,TARIKI 10/10/2011 BAADA YA MAFUNGO MAKUBWA YA SIKU TATU KWA WACHAGULIWA WOTE ULIMWENGUNI.